Katika mwaka wa 2023, dunia ilishuhudia viwango vipya vya juu vya uzalishaji wa gesi ya ukaa, hali ya joto ikiyumbayumba na athari za mabadiliko ya tabianchi kushuhudiwa kwa kishindo na kwa kasi zaidi.
Wakati uo huo, mengi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yako mbali kufikia nusu ya Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.
Licha ya haya yote, mwitikio wa kimataifa kwa changamoto za aina tatu duniani za janga la mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai, uchafuzi na taka viliongezeka. UNEP ilitekeleza wajibu muhimu kwa kutoa sayansi muhimu na masuluhisho kuhusiana na changamoto za aina tatu duniani, kuitisha na kuwezesha mazungumzo, kuandaa mikataba muhimu ya kimataifa ya mazingira, kufanya kazi na watu binafsi na sekta za fedha ili kuoanisha ufadhili na michakato ya kimataifa na kusaidia Nchi Wanachama kutekeleza ahadi zao. Soma zaidi katika ripoti ya kila mwaka ya mwaka huu.