19 December 2022 Ripoti

Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal

Waandishi: CONVENTION ON BIOLOGICAL DIVERSITY (CBD)
Jalada

Kuitimika kwa Kongamano la 15 la Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkataba wa Uanuai wa Kibayolojia kulipelekea kupitishwa kwa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal (GBF)

Huku kukiwa na uharibifu mbaya wa mazingirak unaohatarisha maisha ya viumbe milioni 1 na kuathiri maisha ya mabilioni ya watu, GBF inalenga kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mazingira.  Mfumo huu una malengo ya kimataifa yanayotarajiwa kufikiwa kufikia mwaka wa 2030 na badaye ili kulinda na kutumia bayoanuwai kwa uendelevu.

Kwa kuwa kwa sasa mfumo huu umepitishwa, kuimarisha hatua katika sekta mbalimbali na katika jamii ili kufikia malengo na shabaha za GBF ni muhimu kushughulikia vyanzo vikuu vya uharibifu wa bayoanuai na kupika jeki ajenda ya mazingira.

Malengo makuu manne yanayohitaji kufikiwa kufikia mwaka wa 2050 yanazingatia ubora wa mifumo ya ekolojia na afya ya viumbe ikijumuisha kuangamia kwa spishi kutokana na shughuli za binadamu, matumizi endelevu ya bayoanuai, mgao sawa wa faida, na kuhusu utekelezaji na ufadili kujumuisha kuziba pengo la ufadhili wa bayoanuai la dola bilioni 700 kila mwaka.

Miongoni mwa malengo ishirini na tatu yanayopaswa kufikiwa kufikia mwaka wa 2030 ni pamoja na asilimia 30 ya uhifadhi wa ardhi na bahari, asilimia 30 ya ureshaji wa mifumo ya ekolojia iliyoharibiwa, kupunguza kwa nusu kuanzishwa kwa spishi vamizi, na kupunguza dola bilioni 500 kwa mwaka kwa ruzuku inayodhuru.

#COP15: Ni wakati wa kuimarisha juhudi

Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (COP15) lilimalizika mjini Montreal, Canada, tarehe 19 Disemba mwaka wa 2022 na makubaliano ya kihistoria ya kuongoza hatua za kimataifa za kushughulikia mazingira hadi mwaka wa 2030.  Ikiongozwa na China huku Canada ikiwa mwenyeji, COP 15 ilipelekea kupitishwa kwa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal (GBF).

Viongozi wachunguza jinsi ya kushiriki kwa usawa manufaa ya mazingira

Wanasiasa, wanasayansi na wanaharakati wa mazingira wanakusanyika mjini Montreal, Kanada, wiki hii kwa mazungumzo kuhusu mpango wa kimataifa wa kulinda bayoanuai inayopungua duniani.  

 

Hali ya Ufadhili wa Mazingira 2022

Toleo la pili la ripoti ya Hali ya Ufadhili wa Mazingira iliyozinduliwa leo inaonyesha kuwa masuluhisho ya kiasili bado hayapati ufadhili wa kutosha. Iwapo dunia inataka kukomesha uharibifu wa bayoanuai, kudhibiti mabadiliko ya tabianchi yasizidi nyuzijoto 1.5 na kufikia kutokuwa na uharibifu wa ardhi kufikia mwaka wa 2030, mtiririko wa sasa wa fedha kwa NbS lazima uimarishwe dufu…