Kushiriki kwa Mashirika ya Uraia
Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linatambua umuhimu wa kushirikisha Makundi Makuu mbali na Wadau wengine kama washirika na kujivunia mielekeo wanayoleta, tafiti muhimu na uhamasishaji wanaofanya na wajibu wao wa mda mrefu, ulio mpana wa kuunga mkono dhamira ya UNEP.
Uamuzi unaofanywa na serikali mbalimbali utatamba kote, kuimarika na kuungwa mkono na serikali iwapo maoni ya Makundi Makuu na Wadau yatazingatiwa mapema ipasavyo wakati wa michakato ya kutunga sera na kufanya mauamuzi. Makundi Makuu na Wadau pia huwa mstari mbele wakati wa utungaji sera; wao hufanya kazi kama watafiti, washauri, wanaharakati au wahamasishaji.
Kujenga Ushirikiano Mzuri Kikamilifu kati ya Makundi Makuu na Wadau(MGS) na UNEA 5.2 na UNEP Webinar ya UNEP MGS - Kuwajengea Uwezo wa UNEA 5.2
Kuandaa Makundi Makuu na Wadau (MGS) kushiriki kikamilifu kwenye UNEA 5.2, kwa msaada wa UNEP, Jukwa la Wadau wa Mustakabali Endelevu (https://stakeholderforum.org/) liliandaa msururu wa mafundinzo kwa kanda zote sita miezi minne mwishoni mwa mwaka wa 2021.
Makala kwenye lugha za Kiarabu, Kifaransa, na Kihispania ya webinar hizo zilizorekodiwa yanapatikana mbali na ya Kiingereza. Makala yaliyorekodiwa ya webinar zote tano yanaweza patikana kwenye wavuti ya Jukwa la Wadau wa Mustakabali Endelevu ukrasa wa Webinar za SF.
Mawasilisho kwa lugha ya Kiingereza na Kihispania yako tayari, tafsiri ya Kifaransa itakuwa tayari hivi karibuni.
UNEP@50 na UNEP Tunayotaka