Lini: Julai 8 - 17, 2024
Wapi: New York, Marekani
Taarifa kuhusu kujisajili na kushiriki
Kongamano la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu (HLPF) litafanyika kuanzia Jumatatu, tarehe 8 Julai, hadi Jumatano, tarehe 17 Julai mwaka wa 2024, chini ya usimamizi wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC). Hii inajumuisha awamu ya siku tatu ya mawaziri katika kongamano kuanzia Jumatatu, tarehe 15 Julai, hadi Jumatano, tarehe 17 Julai mwaka wa 2024 kama sehemu ya Awamu ya Ngazi ya Juu ya Baraza. Siku ya mwisho ya Awamu ya Ngazi ya Juu ya ECOSOC itakuwa Alhamisi, tarehe 18 Julai mwaka wa 2024.
Kaulimbiu itakuwa "Kuimarisha Ajenda ya 2030 na kutokomeza umaskini wakati wa majanga anuai: utoaji mwafaka wa masuluhisho endelevu, thabiti na bunifu".
Mpango wa HLPF utajumuisha upitiaji wa mada za Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 1 ya kukomesha umaskini, 2 juu ya kutokomeza njaa, 13 kuhusu hatua kwa tabianchi, 16 kuhusu amani, haki na taasisi thabiti, na 17 kuhusu ushirikiano wa Malengo.
HLPF ya 2024 itasaidia utekelezaji wa Azimio la Kisiasa na matokeo mengine ya Kongamano la SDG la mwaka wa 2023 ya kuendeleza Ajenda ya 2030 na SDGs.
Hafla zingine, ikijumuisha Hafla za Kando, VNR Labs, Hafla Maalum, na Maonyesho zitaendeshwa wakati wa HLPF ya mwaka wa 2024.