Picha: Unsplash/Petr Magera
21 Jul 2022 Video Miji

Kutumia kilimo mijini kuimarisha miji

Miji, ambayo hukalia asilimia 3 tu ya ardhi Duniani, huchangia hadi asilimia 80 ya matumizi ya nishati na asilimia 75 ya uzalishaji wa gesi ya ukaa. Kufikia mwaka wa 2050, takribani  asilimia 70 ya watu duniani wanatarajiwa kuishi mijini, jambo ambalo wataalam wanaonya kuwa litasababisha mabadiliko makubwa zaidi ya mazingira na kuchangia kwa changamoto za aina tatu duniani. Ili kushughulikia masuala yanayohusiana na ukuaji wa haraka wa miji, serikali lazima zichukue hatua madhubuti ili kujenga miji thabiti na endelevu.

Kuhakikisha kuna utoshelezaji wa chakula mijini na kupunguza shinikizo kwa afya ya binadamu na kwa mazingira ni changamoto kuu ambayo miji inakabiliana nayo - na kilimo cha mijini kinaweza kuwa mojawapo ya masuluhisho yanayohitajika.

Kutumia tena rasilimali za mijini na kukuza kilimo mijini kuna manufaa mengi kwa afya, kwa jamii na kwa uchumi. Kunaweza pia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na uharibifu wa bayoanuai, na uchafuzi na taka, kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Ukuzaji wa chakula karibu na watumiaji wake hupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa unaohusishwa na usafirishaji na uhifadhi, huumarisha uwezo wa kufikia lishe bora na kufanya mifumo ya chakula kuwa dhabiti.

Kupitia usimamizi dhabiti wa kitaasisi, miji inaweza kukumbatia mifumo ya chakula inayotumia bidhaa tena na zaidi ili kulinda afya ya binadamu na mazingira.

https://www.youtube.com/watch?v=N7-mNylq4Ok&ab_channel=UNEnvironmentProgramme

 

Maudhui Yanayokaribiana