Tuzo la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.
UNEP inatafuta kupendekezwa kwa watu binafsi na mashirika yanayofanya kazi kupata masuluhisho bunifu na endelevu ya kuboresha ardhi, kuimarisha ustahimilivu kwa ukame, na kupambana na kuenea kwa majangwa.
Upendekezaji wa wawaniaji wa awamu ya mwaka wa 2024 unaendelea kwa sasa
.
Upendekezaji unaweza kufanywa katika viwango vinne
Mchakato wa kuchaguliwa
Wafanyakazi wa UNEP na wataalam wa mada husika huchagua kutoka kwa orodha ya mapendekezo yaliyopokelewa kutoka kote duniani. Mtu yeyote anaweza kutoa mapendekezo/kupendekezwa. Katika mwaka wa 2023, UNEP ilipokea mapendekezo 2,500, na kuwa mwaka wa tatu mfululizo wa kupokea mapendekezo mengi zaidi.
Vigezo vya kuchaguliwa ni kama vifuatavyo:
- Athari: Je, juhudi za aliyependekwa zimepelekea manufaa makubwa ya kimazingira au zimeonyesha kuwa na uwezekano mkubwa wa kurudufishwa na kuimarishwa zaidi?
- Mambo mapya: Je, aliyependekezwa amefanya au kupelekea kitu kipya na bunifu?
- Ushawishi: Kisa cha aliyependekezwa kinavutia kwa kiwango kipi?