-
Uzalishaji wa gesi ya ukaa kutoka kwa sekta ya kupunguza joto unatabiriwa kuongeza maradufu kufikia mwaka wa 2050
-
Hatua muhimu zinaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa nishati, kupunguza uzalishaji wa hewa chafu uliotabiriwa kwa asilimia kati ya 60 na 96
- Watu bilioni 3.5 wanatarajiwa kunufaika kutokana na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kupunguza joto
Dubai, Desemba 5, 2023 – Kuchukua hatua muhimu za kupunguza matumizi ya umeme ya vifaa vya kupunguza joto kunaweza kupunguza angalau asilimia 60 ya uzalishaji wa hewa chafu uliotabiriwa kwa kuzingatia sekta kufikia mwaka wa 2050, kuwezesha kufikiwa kwa vifaa muhimu vya kupunguza joto na watu wote ulimwenguni wa kuweza kuokoa maisha, kuondoa shinikizo kwa mitambo ya kutoa nishati na kuokoa matrilioni ya dola kufikia mwaka wa 2050, kulingana na ripoti mpya iliyochapishwa wakati wa mazungumzo ya mazingira ya COP28 mjini Dubai.
Ripoti hii, Kudumisha Ubaridi: Jinsi ya kukidhi mahitaji ya kupunguza joto huku tukipunguza uzalishaji wa hewa chafukutoka kwa muungano wa kupunguza joto wa Cool Coalition, inaainisha hatua endelevu katika maeneo matatu: mifumo ya kupunguza joto isiyohitaji ukarabati, viwango bora vya kutumia nishati vizuri kuundia vifaa vya kupunguza joto na hatua za dharura za kuachana na friji zinazoongeza joto. Kufuata hatua zilizoainishwa katika maeneo haya kunaweza kupunguza hewa chafu kwa asilimia 60. Kuongeza kutumia mifumo ya nishati isiozalisha hewa ya ukaa kutapunguza uzalishaji wa hewa chafu kuzingatia sekta kwa asilimia 96.
Ripoti hii inayotolewa ili kuunga mkono Ahadi za Kupunguza Joto Duniani, mpango wa pamoja kati ya Muungano wa Cool Coalition na Umoja wa Falme za Kiarabu kama mwenyeji wa COP28. Leo, nchi zaidi ya 60 zilitia saini ahadi zinazoonyesha kujitolea kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kutoka kwa sekta ya kupunguza joto.
“Kadiri joto linavyoongezeka, ni muhimu kushirikiana kuboresha ufanisi wa nishati na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa sekta ya kupunguza joto huku tukiimarisha upatikanaji wa vifaa endelevu kupunguza joto. Ufikiaji huu ni muhimu hasa kwa jamii zilizo hatarini zaidi, ambazo mara nyingi huchangia kiwango kidogo zaidi cha mabadiliko ya tabianchi lakini ndizo zinazoathiriwa zaidi,” alisema Dk. Sultan Al Jaber, Rais wa COP28.
"Sekta ya kupunguza joto ni sharti ikue ili kulinda kila mtu dhidi ya ongezeko la joto, kudumisha ubora na usalama wa chakula, kuweka chanjo kwa njia thabiti na kukuza chumi," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji of UNEP. "Bali ukuaji huu haupaswi kutokea kwa kugharimu mabadiliko ya nishati na kuzidisha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi. Mataifa na sekta ya kupunguza joto ni sharti wachukue hatua sasa ili kuhakikisha sekta ya kupunguza joto inakua kwa kupunguza hewa ya ukaa. Kwa bahati nzuri, masuluhisho yanapatikana sasa. Kwa kutumia nishati vizuri, haki ya kupunguza joto kwa njia endelevu kunatoa fursa ya kupunguza ongezeko la joto duniani, kuboresha maisha ya mamilioni ya watu, na kuwa na akiba kubwa ya fedha."
Ukuaji wa haraka na usio endelevu wa vifaa vya kupunguza joto
Mabadiliko ya tabianchi, ukuaji wa idadi ya watu na mapato, na ujenzi wa miji unaongeza mahitaji ya kupunguza joto, ambayo ni muhimu ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Takriban watu bilioni 1.2 barani Afrika na Asia wanakosa huduma za kupunguza joto - na hivyo kuhatarisha maisha kutokana na joto kali, kupunguza mapato ya wakulima, kupelekea uharibifu wa chakula, na kuzuia upatikanaji wa chanjo kwa wote.
Tukiendelea na mfumo wetu wa kufanya maendeleo kwa sasa, vifaa vya kupunguza joto vinawakilisha asilimia 20 ya jumla ya matumizi ya umeme kwa sasa – na inatarajiwa kuongezeka zaidi ya maradufu kufikia mwaka wa 2050. Uzalishaji wa gesi ya ukaa kutokana na matumizi ya umeme utaongezeka, mbali na gesi inayovuja kutoka kwa friji, ambayo nyingi yake ina uwezo mkubwa wa kuongeza joto duniani kuliko kaboni dioksidi. Tukiendelea na mambo kama kawaida, uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa vifaa vya kupunguza joto unakadiriwa kuchangia kwa zaidi ya asilimia 10 ya uzalishaji wa hewa chafu ulimwenguni kufikia mwaka wa 2050.
Kuongezeka kwa mahitaji ya vifaa vya bei nafuu lakini visivyokuwa bora, ikiwa ni pamoja na viyoyozi na friji, kutahitaji uwekezaji mkubwa katika miundomsingi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme. Vifaa visivyokuwa bora pia vitasababisha kodi ya juu ya umeme kwa watumiaji, haswa barani Afrika na Asia Kusini, ambapo ukuaji wa haraka zaidi unatabiriwa.
"Sekta ya kibinafsi ina wajibu mkuu wa kutekeleza katika ufadhili na kuendesha uvumbuzi ili kupunguza joto kwa njia endelevu, hali inayoweza kusaidia kutimiza mahitaji muhimu ya maendeleo ya eneo na kusaidia malengo ya kimataifa ya kupunguza gesi ya ukaa. Tunafurahi kuchangia Ripoti ya Tathmini ya Kimataifa ya Kupunguza Jotona kuunga mkono Ahadi za Kupunguza Joto Duniani,” alisema Makhtar Diop, Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Fedha la Kimataifa.
Manufaa kwa mazingira, afya ya binadamu na ustawi.
Kufuata mapendekezo ya ripoti hii kunaweza kupunguza makadirio ya uzalishaji wa hewa chafu kufikia mwaka wa 2050 tukiachana na mifumo ya kawaida ya kupunguza joto kwa zaidi ya asilimia 60 – karibu tani bilioni 3.8 za CO2e.
Hii inaweza:
- Kuruhusu watu bilioni 3.5 zaidi kunufaika na friji, viyoyozi au vifaa vya kupunguza joto visivyohitaji ukarabati kufikia mwaka wa 2050.
- Kupunguza kodi za umeme kwa watumiaji kwa dola za Marekani trilioni 1 kufikia mwaka wa 2050, na kwa jumla dola za Marekani trilioni 17 kati ya mwaka wa 2022 na 2050.
- Kunguza mahitaji ya juu ya nishati kwa kati ya terawati (TW) 1.5 na 2 – karibu maradufu ya jumla ya uwezo wa uzalishaji wa EU kwa sasa.
- Kuepuka uwekezaji wa kuzalisha umeme wa kiasi cha dola za Marekani kati ya trilioni 4 na 5.
Kujumuisha uondoaji wa gesi ya ukaa kwa nishati kunaweza kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kwa asilimia 96. Nchi za G20 zinawakilisha uwezekano wa asilimia 73 ya ukupunguza uzalishaji wa hewa chafu kufikia mwaka wa 2050.
Ripoti inaelezea hatua muhimu za kuchukua katika mikakati ya kupunguza joto bila ukarabati kuhitajika, viwango bora vya kutumia nishati vizuri na kupunguza kwa kasi friji za hydrofluorokaboni (HFC) zinazoongeza joto kupitia Marekebisho ya Kigali ya Mkataba wa Montreal.
Kufikia mwaka wa 2022, zaidi ya asilimia 80 ya nchi zilikuwa na angalau chombo kimoja cha kisheria cha kushughulia maeneo haya, lakini utekelezaji bado hautoshi. Ni asilimia 30 pekee ya nchi zina sheria zinazowezesha kuchukua hatua katika nyanja zote tatu.
Hatua za kupunguza joto bila kuhitaji ukarabati
Hatua za kupunguza joto bila kuhitaji ukarabati – kama vile kuhami, vivuli asilia, uingizaji hewa na maeneo yanayoakisi – zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kupunguza joto. Haya yanawezekana, kwa kiasi fulani, kupitia ukuzaji na utekelezaji wa mifumo ya ujenzi ya kupunguza joto bila kuhitaji ukarabati, na muundo wa miji.
Mikakati kama hii inaweza kuzuia ukuaji wa mahitaji ya uwezo wa kupunguza joto kufikia mwaka wa 2050 kwa asilimia 24, na kusababisha kupunguza gharama ya mtaji kupitia kutohitaji vifaa vipya vya kupunguza joto vya hadi Dola za Marekani trilioni 3, na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kwa tani bilioni 1.3 za CO2e.
Viwango bora vya kiwango cha juu
Viwango bora vya juu vya na uwekaji wa lebo bora wa vifaa vyote vya kupunguza joto vitaongeza mara tatu wastani wa ufanisi wa kimataifa wa vifaa vya kupunguza joto kufikia mwaka wa 2050 kutoka kwa viwango vya sasa, na kupelekea kuokoa kwa umeme kwa asili 30, kupunguza kodi ya umeme na kuboresha uthabiti na uwezo wa kifedha wa mitambo ya kuongeza baridi.
Sera muhimu za utekelezaji ni pamoja na Viwango vya Kima cha Chini cha Utendakazi (MEPS) vinavyosasishwa mara kwa mara, mbinu za kifedha za kuhimiza mahitaji ya bidhaa za ngazi ya juu zaidi ili kuepuka utupaji wa vifaa duni vya kupunguza joto kwa nchi zinazoendelea.
Marekebisho ya Kigali
Ulimwengu umejitolea kupunguza HFCs kupitia Marekebisho ya Marekebisho ya Kigali kwa Mkataba wa Montreal - makubaliano ya kimataifa yaliyoundwa kulinda tabaka la ozoni na kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi.
Uzalishaji wa HFC kufikia mwaka wa 2050 unaweza kupunguzwa kwa nusu kulingana na ratiba ya Kigali ya upunguzaji kupitia utumiaji kwa kasi wa teknolojia bora katika vifaa vipya, na usimamizi bora wa friji, pamoja na utekelezaji thabiti wa kitaifa.
Ufadhili ni muhimu
Zana za kifedha ni pamoja na ufadhili wa kulipia kila mwezi (wakati shirika linapolipia uboreshaji na kurejeshewa pesa kupitia kodi za umeme za kila mwezi), vifaa vya kugawana madhara, uwekezaji wa umma na wa kibinafsi, rehani zisizochafua mazingira, kujumuisha upunguzaji joto kwa njia endelevu katika ulinzi wa ESG kwa benki za kimataifa, na kulinda wakulima wadogo katika nchi zinazoendelea kwa kupitia mtaji wa hisa. Kwa nchi nyingi zinazoendelea, ufadhili wa masharti nafuu vitahitajika.
MAKALA KWA WAHARIRI
Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
Kuhusu Muungano wa Cool Coalition
Muungano wa Cool Coalition unaoongozwa na UNEP ni muungano wa kimataifa wa washikadau mbalimbali unaleta pamoja wahusika mbalimbali wakuu kutoka serikalini, mijini, mashirika ya kimataifa, mashirika ya biashara, mashirika ya fedha, wasomi na mashirika ya uraia ili kuwezesha kubadilishana maarifa, kufanya uhamasishaji na kuchukua hatua za pamoja za kuwezesha kuwa na mabadiliko ya haraka ya kimataifa ya kupunguza joto kwa njia endelevu. Muungano wa Cool Coalition kwa sasa unafanya kazi na zaidi ya wabia 130, zikiwemo nchi 23. Muungano wa Cool Coalition ni mojawapo ya matokeo rasmi na "Mipango ya Mabadiliko" iliyowekwa na Ofisi ya Tendaji ya Katibu Mkuu kwa Mkutano wa Kilele wa Ushughulikiaji wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa mwaka wa 2019 na mshirika wa utoaji wa huduma za kiufundi kwa Urais wa COP28 wa UAE kuhusu Ahadi za Kupunguza Joto Duniani.
Kuhusu Ahadi za Kupunguza Joto Duniani
Ahadi za Kupunguza Joto Duniani ni fursa ya kujitolea kupunguza joto kwa njia endelevu kwa kuchukua hatua madhubuti. Mpango wa Umoja wa Falme za Kiarabu kama mwenyeji wa Kongamano la mwaka wa 2023 la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), Ahadi hii ni mojawapo ya matamko, ahadi na mikataba tisa muhimu ambayo ni matokeo muhimu ya Ajenda ya Utekelezaji ya Rais wa COP28. Inalenga kuimarisha ahadi na ushirikiano wa kimataifa kupitia malengo ya pamoja ya kimataifa ili kupunguza uzalishaji wa hewa chafu unaohusishwa na mitambo ya kupunguza joto kwa asilimia 68 kuanzia sasa hadi mwaka wa 2050, kuimarisha kwa kiasi kikubwa ufikiaji wa vifaa vya kudumu vya kupunguza joto kufikia mwaka wa 2030, na kuongeza wastani wa ufanisi wa kimataifa wa viyoyozi vipya kwa asilimia 50. Malengo ya uzalishaji wa hewa chafu yanaigwa kutoka kwa ripoti ya UNEP na Cool Coalition ya Kudumisha Ubaridi: Jinsi ya kukidhi mahitaji ya kupunguza joto huku tukipunguza uzalishaji wa hewa chafu.
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Kitengo cha Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa